TAMWA YAAZIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

08 March 2017 Written by 
Published in PRESS RELEASE
Chama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA kinaungana na mashirika yanayotetea haki za binadamu hasa wanawake na watoto ulimwenguni kusherekea siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa tarehe 8 mwezi Machi kila mwaka.   Kauli mbiu kitaifa mwaka huu ni “Tanzania ya Viwanda: Mwanamke ni Msingi wa Mabadiliko Kiuchumi” ambayo inatutaka wote tushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya mitazamo, fikra na matarajio ya kimaendeleo hasa kwa wanawake. Aidha kauli mbiu ya mwaka huu inatazamia serikali na wanasheria kuboresha sera na sheria ili ziweze kuleta uwezo wa ustawi na kuwawezesha wanawake wawe na uwezo wa kufikia mabadiliko yao ndani ya familia  na kuleta usawa katika maamuzi .   Inakadriwa kuwa duniani kote ni asilimia 50 tu ya wanawake ambao wanajishugulisha na kazi rasmi ikilinganishwa na asilimia 76 ya wanaume. Aidha kazi nyingi ambazo zimekuwa zikifanywa na wanawake ni za hali ya chini na zinawaingizia kipato duni.   TAMWA inaamini kuwa azma ya nchi ya kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati na viwanda  itafikiwa endapo haki ya elimu kwa mtoto wa kike itapewa kipaumbele na kuhakikisha sera na sheria kandamizi kwa wanawamke na watoto wa kike zitarekebishwa na kuwezesha ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi mbalimbali za uongozi na maamuzi.   Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yana lengo la kuwezesha jamii kupima utekelezaji wa maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbalimbali za Kimataifa/ kikanda  na kitaifa zinazohusu masuala ya maendeleo ya jinsia na wanawake katika kuhakikisha haki za wanawake kiuchumi, kijamii, na kisiasa zinapatikana na zinalidwa.   Edda Sanga Mkurugenzi Mtendaji
Read 23919 times Last modified on Wednesday, 08 March 2017 05:37
Rate this item
(0 votes)

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

July 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper