Wabunge wa Bunge la Tanzania leo tarehe 26 Juni, 2016 wameunga mkono juhudi za TAMWA katika uhamasishaji umma kuhusu matatizo yaliyopo kwenye matumizi ya pombe kupita kiasi na madhara yake kiafya na kijamii. Hayo yamezungumzwa leo hii katika mkutano kati ya wabunge na waandishi wa habari kama ulivyoandaliwa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania –TAMWA. 

 

Mkutano huo uliochukua sura ya pekee, kwa kuwa na mada nne (4) zilizowasilishwa ikiwemo iliyohusu masuala ya ukatili wa kijinsia, sheria za pombe zilizopo nchini, madhara ya pombe na ongezeko la magonjwa ya akili na madhara ya pombe na afya ya Jamii nchini.

 

Wabunge kwa umoja wao walikiri kuwa pamoja na changamoto zilizopo, na kusema kuwa nchini kwetu, pombe aina ya viroba imekuwa ni changamoto kubwa ambapo mbali na kuharibu akili za vijana pia vinachafua mazingira.

 

Aidha, Mwenyekiti wa vikao vya Bunge na Mbunge wa Ilala Mheshimiwa Zungu alikiri kuwa, pombe ni adui ambaye anatakiwa kudhibitiwa, na kufananisha hata uwepo wa majanga kama vile ndoa za umri mdogo kufananisha na maamuzi yanayo amuliwa kwenye vikao vya pombe.

 

Mkutano huu ulifanyika katika ukumbi wa Bunge, Msekwa D. mjini Dodoma, ulikutanisha  wajumbe wa kamati tatu ambazo ni Sheria ndogondogo, kamati ya Maendeleo ya Jamii Mipango na ile inayohusika na Serikali za Mtaa. Mkutano huu umefanikiwa kutokana na ufadhili wa IOGT-NTO Movement.

WABUNGE WAIPONGEZA TAMWA

FLAT YENYE VYUMBA VIWILI, SEBULE, MALIWATO NA JIKO INAPANGISHWA KWA BEI NAFUU. IPO KISUTU SOKONI. MAWASILIANO PIGA: 0222772681 AU 0222771005 AU 0754285701

FLAT INAPANGISHWA

Imetolewa Tar 4/8/2016.

Tumekusanyika hapa leo kuonyesha kushangazwa na kusikitika kwetu baada ya kuona taarifa iliyotolewa na mwanasheria mkuu wa Serikali ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani ili kupinga maamuzi yaliyotolewa na Mahakama Kuu.

TAMKO LA MTANDAO WA KUPINGA NDOA ZA UTOTONI TANZANIA KUHUSU NIA YA MWANASHERIA MKUU KUKATA RUFAA

Katika kuadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani ambayo huadhimishwa tarehe 11 Oktoba ya kila mwaka, wafanyakazi wa Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) wamevitembelea  baadhi ya vyombo vya habari nchini. Lengo kubwa likiwa ni kuwapongeza wanahabari kwa namna  wanavyoibua na kuandika habari za ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto pamoja na  kutoa elimu kwa jamii kuhusu haki za watoto, jambo  ambalo limewafungua wananchi kuona ni hatua zipi za kuchukua pindi wanapoona vitendo hivyo katika jamii au familia vinatokea.

Mbali na pongezi, TAMWA wanavipongeza vyombo vya habari vyote nchini kutokana na kuweza kutoa nafasi kubwa kuchapisha habari za ukatili wa kijisia kwa wingi na hata kuzipa uzito wa kuzichapisha  katika kurasa  za mbele tofauti na miaka ya nyuma.

TAMWA KUTEMBELEA VYOMBO VYA HABARI

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzani - TAMWA leo kimeungana na mashirika yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto hasa watoto wa kike.

 

Kauli mbiu ya mwaka huu, ya “Funguka! Pinga Ukatili wa Kijinsia: Elimu Salama Kwa Wote”, inalenga kila mzazi, mlezi, ndugu, jamaa kwa kushirikiana na serikali kumlinda mtoto hasa wa kike katika kumhepusha na vizuizi ili aweze kufikia ndoto zake.

TAMWA YAUNGANA NA WADAU WA KUTETEA HAKI ZA WANAWAKE NA WATOTO KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA.

Wanasheria na Maafisa ustawi wa jamii wa Kituo cha usuluhishi TAMWA leo tarehe 7/12/2016 wametembelea kata ya Makumbusho maeneo ya Mwananyamala kwa Mwinjuma kwa ajili ya kutoa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahitaji wa msaada huo . Ikiwa ni maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia .

Msaada huo ulitolewa kwa watu 15 kwa wakazi wa eneo hilo ambapo waliweza kusaidiwa. Mashauri mengi yaliyoletwa mbele ya Kituo cha usuluhishi TAMWA ni ya ndoa, matunzo, ardhi, mirathi na madai.

Msaada wa kisheria na ushauri nasihi uliambatana na utoaji wa elimu kwa wakazi wa Mwananyamala kuhusu sheria mbalimbali jinsi ya kutoa taarifa na wapi pa kupeleka taarifa wakiwa wanahitaji msaada wa kisheria.

Kituo cha usuluhishi bado wanaendelea kutoa msaada wa kisheria na ushauri nasihi katika Ofisi zao zilizopo TAMWA – Sinza Mori.

TAMWA WAADHIMISHA SIKU YA MSAADA WA KISHERIA KWA KUTOA MSAADA WA KISHERIA NA USHAURI NASIHI KATIKA KATA YA MAKUMBUSHO, WILAYA YA KINONDONI, DAR ES SALAAM

Chama Cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) leo kimeanza mkutano wake wa siku mbili kupanga mpango kazi wa mwaka 2017 ili kuhakikisha wanawafikia wanawake na watoto. Pia kujitathmini katika mafanikio na changamoto walizokutana nazo najinsi walivyozimaliza.

Mkutano unafanyika katika ukumbi wa mkutano kibaha (kibaha conference center) na umehudhuriwa na wafanyakazi wote wa chama hicho wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA Bi Edda Sanga.

TAMWA YAJIPANGA KWA MWAKA 2017

Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kupitia kitengo chake cha usuluhishi na ushauri nasihi (Crisis Resolving Center – CRC), leo kimehudhuria na kutoa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa watu waliohudhuria maazimisho ya siku ya ustawi wa jamii duniani.

Maadhimisho hayo yameyofanyika  katika viwanja vya Taasisi ya Ustawi wa Jamii iliyoko Kijitonyama, jijini Dar es Salaam. Akiongea katika maadhimisho hayo, Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mh. Hamisi Kigwangala, amesema kuwa ni wakati sasa kwa Wataalam wa ustawi wajamii kupitia wizara hiyo kuwa na sheria  ya kitaaluma ya ustawi, ambapo amemwagiza katibu mkuu wa wizara yake kuhakikisha mswada huo kufikishwa bungeni mwaka huu mwezi wa tisa ili upitishwe na kuwa sheria.

Waziri Kigwangala amesema kwa sasa kumekua na mmomonyoko wa maadili, zikiwemo mimba za utotoni, utumiaji wa madawa ya kulevya, mapenzi ya jinsia moja, ubakaji pamoja na ulawiti. Aidha amewataka Maafisa ustawi wa jamii kuendelea kusimamia na kuelimisha Jamii kuhusiana na ongezeko la vitendo viofu katika jamii.

Kauli mbiu ya siku hii ni, “USTAWI WA JAMII: KUKUZA NA KUIMARISHA JAMII NA MAZINGIRA”.

SIKU YA USTAWI WA JAMII DUNIANI (WORLD SOCIAL WORK DAY) TAREHE 21 MACHI 2017

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), kimekutana na wahariri kutoka Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam kujadili namna ya kuripoti habari zinazohusu masuala ya usalama barabarani.

Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA Bi Edda Sanga , amewashukuru wahariri kwa ushirikiano mkubwa waliotoa wakati wa utekelezaji wa mradi wa Usalama Barabarani awamu ya kwanza ambao ulichukua miezi saba kukamilika. Pia aliwaomba kuanza kwa pamoja utekelezaji wa awamu nyingine ya mradi mpya ambao utahusisha mikoa ya Pwani, Morogoro na Dar es Salaam.

Kwa kauli moja wahariri waliridhia kutoa ushirikiano wa dhati kwa kuandika na kurusha habari zenye kulenga kushawishi maboresho ya sheria ya sasa ya Usalama Barabarani ya mwaka 1973 na pia kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya sheria na kanuni za usalama barabarani.

TAMWA YAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI

Balozi wa Dernmark (Bwana Einar Jensen) na Mkurugenzi wa Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania – TAMWA (Bibi Edda Sanga), wamesaini mkataba mpya wa miaka mitano (2017 – 2021) wenye lengo la kuihamasisha jamii kujenga na kuimarisha haki na usawa wa kijinsia ili kutokomeza ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto hapa nchini.

TAMWA imekuwa ikitekeleza mradi huo kwa ufadhili wa DANIDA kuanzia tarehe 30 October 2012.

DANIDA NA TAMWA WASAINI MKATABA MPYA

Wanafunzi wa shule ya Kimataifa ya Dar es Salaam International Academy wametembelea Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa lengo la kujifunza umuhimu wa vyombo vya habari katika kutetea haki za wanawake na watoto katika jamii.

Wanafunzi hao walipokelewa na Afisa wa kitengo cha jinsia TAMWA, Bi Godfrida Jola na kuwaeleza  maana halisi ya ukatili wa kijinsia pamoja na vitendo wanavyofanyiwa watoto na wanawake katika jamii vinavyokiuka haki zao za msingi na kupelekea ukatili wa kijinsia.  

Pia walielezwa  ni kwa jinsi gani vyombo vya habari vinavyoweza kuwa chachu ya kumaliza ukatili wa kijinsia kupitia kalamu zao na vipindi vya  redio vya kuelimisha jamii.

Wanafunzi hao walipata fursa ya kuuliza maswali na kujionea kazi  mbalimbali zinazofanywa na TAMWA katika kupambana na ukatili wa kijinsia unaoendelea katika jamii mbalimbali hapa nchini.

WANAFUNZI WA SHULE YA DAR ES SALAAM INTERNATIONAL ACADEMY WATEMBELEA TAMWA

Mapendekezo ya Maboresho ya Sheria ya Usalama Barabarani kwa mtazamo wa visababishi vitano vya ajali

Mtandao wa wadau kutoka Asasi za Kiraia unaotetea Marekebisho ya Sheria na Sera inayohusu Usalama Barabarani Tanzania, umeungana na watanzania katika Maadhimisho ya Nne ya Umoja wa Mataifa ya Wiki ya Usalama Barabarani (UN Road Safety Week) yalionza tarehe 08/05/2017 na kufikia kilele chake tarehe 14/05/2017. Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Udhibiti wa Mwendo Kasi kwa Vyombo vya Usafiri”.

Wakati tunaadhimisha Wiki ya Umoja wa Mataifa ya Usalama Barabarani, tumeshuhudia matukio mbalimbali ya ajali ambazo chanzo chake kikubwa ni makosa ya kibinadamu. Mfano mmojawapo ni ule wa tukio la tarehe 6 Mei mwaka huu, ambapo taifa letu  lilipatwa na simanzi, pale wanafunzi 33 na walimu wao wawili pamoja dereva walipata ajali na kufariki papo hapo katika wilaya ya  Karatu, Mkoani Arusha.

Kama sehemu mojawapo ya Maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa ya Usalama Barabarani, Mtandao wa wadau kutoka Asasi za Kiraia unaotetea Marekebisho ya Sheria na Sera inayohusu Usalama Barabarani Tanzaniasiku ya tarehe 12 na 13 Mei, 2017 wamefanikiwa kukaa na baadhi ya Wabunge kutoka kamati saba za Bunge. Kamati hizo ni Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Katiba na Sheria, Kamati ya Bajeti, Huduma za Jamii,  Kamati ya Sheria Ndogo, Viwanda na Biashara pamoja na Kamati ya Miundombinu.

Vikao na Kamati hizo viliongozwa chini ya Uenyekiti wa Mwenyeketi wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Balozi Adadi Rajabu ambaye pia ni Mbunge wa Muheza. Katika Vikao hivyo Wabunge  walionyesha dhamira kubwa na kuunga mkono mapendekezo ya kuboresha usalama bararani kwa maendeleo ya Taifa letu.

Wajumbe wa Kamati hizi walipata nafasi ya kusikiliza mada mbalimbali kuhusiana na masuala ya usalama barabarani. Kwa mujibu wa moja ya mada hizo iliyyoelezea hali ilivyo sasa, ilielezwa kuwa madhara yatokanayo na ajali za barabarani yamemeendelea kuwa sababu namba tisa katika kusababisha vifo vya watu wengi zaidi duniani. Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 1.25 hufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani. Wakati huo huo, watu zaidi ya milioni 20 hadi 50 wamebaki na majeraha makubwa na au ulemavu wa kudumu kutokana na ajali hizo kwa mwaka. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa mwaka 2015.

Kwa mujibu ya ripoti ya haki za binadamu kwa mwaka 2016, ajali za barabarani zilipungua katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016, ikilinganishwa na kipindi kama hicho hicho kwa mwaka 2015. Jumla ya ajali 5,152 ziliripotiwa kwa Jeshi la Polisi kuanzia Januari hadi Juni 2016. Pia takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka watu 3,000 hupoteza maisha kutokana na ajali za barabarani Nchini.

Aidha kwa upande wa Tanzania Bara, taarifa kutoka Jeshi la Polisi Kikosi cha  Usalama Barabarani inaonyesha kwamba, kwa mwaka 2016  jumla ya watu 3,256 walipoteza maisha kutokana na ajali za barabarani.  Katika vifo hivyo  wanaume ni 2,580 na wanawake ni 676.  Aidha kumekuwa na majeruhi 8,958 kati  yao wanaume ni 6,470 na wanawake 2,488. Wakati vyombo vya moto vilivyoongoza katika ajali ni magari binafsi ambayo yalisababisha ajali 3,649 ikifuatiwa na pikipiki zilizosababisha ajali 2,544

Kutokana na idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na ajali za barabarani nchini, Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera zinazohusu usalama barabarani Tanzania  umeona  umuhimu na kuchukulia jambo hili na kulifanyia kazi kwa kina. Tafiti zinaonyesha kwamba asilimia 76 ya ajali zote zinatokana na vyanzo vya kibinadamu kama vile Ulevi, Mwendokasi, Uzembe, Uchovu, kupuuzia au kutokuwa makini uwapo barabarani na kutokutii sheria za Usalama Barabarani. Tuna amini matendo haya ya kibinaadamu yanadhibitika kisheria, hivyo basi tunaisihi serikali kuboresha sheria.

Kama wadau wa Usalama Barabarani, tunadhani kuna umuhimu wa sheria sasa kuboreshwa, na hivyo utashi wa kisiasa unatakiwa.  Ndiyo maana tukaitisha majadiliano ya pamoja na Wabunge pamoja na wadau mbalimbali wa Usalama Barabarani ili kuona ni kwa namna gani tunaweza kuleta mabadiliko ya sheria kwa ufanisi na kwa haraka. 

Umoja wa mataifa na Shirika la Afya Duniani wanakiri kwamba sheria  madhubuti zinahitajika katika kupunguza idadi ya watu wanaofariki katika barabara zetu. Tanzania lazima tuwe na sheria kali za usalama barabarani kukomesha hali hii. Katika muda wa miaka mitatu iliyopita Nchi karibia 17 zinazowakilisha wananchi milioni 409 zimetunga na kufanyia maboresho ya sheria angalau kwa kiashiria kimoja au zaidi ambavyo vimekuwa ndio vyanzo vikubwa vya ajali na Nchi hizo zimekuwa zikifanya vizuri katika kudhibiti ajali. TanZania si miongoni mwa nchi hizo. Ni muda mwafaka sasa Tanzania kuchua hatua kwa matendo.

Wabunge waliohudhuria vikao hivi kwa ujumla wao waliona umuhimu wa kuwa na mikakati ya kitaifa ya kupunguza ajali na walionyesha nia na kukubali kuunda Mtandao wa Wabunge wanaotetea usalama barabarani.

Maeneo ambayo tunayapa kipaumbele katika maboresho ya sheria ni kama haya yafuatayo:

a)     Matumizi ya mikanda; Sheria ya sasa ya Usalama barabarani inasema ni kosa kisheria kwa dereva na abiria anayekaa kiti cha mbele kutokufunga mkanda wakati wa safari lakini sheria hiyo hiyo haisemi chochote kwa abiria wanaokaa kiti cha nyuma.

Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) unasema kuwa iwapo ajali ikitokea madhara/athari kwa abiria wa kiti cha mbele itapungua kwa 50% na kwa abiria wa nyuma madhara yatapungua kwa 70%. Kanuni zilizotungwa na SUMATRA zinataka abiria wote wafunge mkanda ila kwa vile sheria mama (Road Traffic Act of 1973) ipo kimya katika eneo hili utekelezaji wa kanuni unakuwa mgumu.

Hivyo basi ni rai yetu sheria hiyo ibadilishwe na kuwataka abiria wote wanaokuwa katika chombo cha usafiri wa kibiashara au binafsi kufunga mkanda wakati wote wa safari.

b)    Matumizi sahihi ya kofia ngumu; Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa ni kosa kwa muendesha pikipiki kutokuvaa kofia ngumu wakati wa kuendesha chombo hicho. Lakini sheria hiyohiyo haisemi chochote kwa abiria anayepanda katika chombo hicho. 

Vilevile pamoja na kuanisha kosa kwa dereva wa pikipiki kutokuvaa kofia ngumu lakini pia sheria haielezi ni jinsi gani kofia inatakiwa kuvaliwa na aina maalum ya kofia inayotakiwa kuvaliwa.

Kwa mujibu wa Utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO)  unaonyesha kuwa iwapo ajali itatokea madhara yanayotokea kwa kutovaa kofia maalum na kwa usahihi ni makubwa sana ukilinganisha na kofia hiyo ikivaliwa  kwa usahihi. Hivyo basi ukizingatia kuwa sasa hivi usafiri wa pikipiki umekuwa unatumika kwa kiasi kikubwa (public transport) hivyo ni rai yetu sheria hiyo ifanyiwe maboresho na kuweka kuwa ni sheria kwa mtu yoyote anayepanda pikipiki kuvaa kofia ngumu na kwa usahihi.

c)     Ulevi: Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa itakuwa kosa kwa mtu yoyote kuendesha chombo cha moto akiwa na kiwango cha kilevi katika damu yake kinachozidi asilimia 0.08% katika mfumo wa mwili. Kiwango hiki ni kikubwa sana kikilinganishwa na tafiti zilizofanywa na Shirika la Afya Duniani na kupendekeza kiwango cha asilimia 0.05% kwa dereva aliyebobea (experienced driver) na asilimia 0.02% kwa dereva  mchanga (young driver). Hivyo basi ni rai yetu kuwa sheria ifanyiwe marekebisho ili iendane na kiwango cha sasa cha kimataifa kilichofanyiwa utafiti.

d)    Mwendo kasi (Speeding): Mwendokasi umeendelea kuwa sababu kubwa ya ajali zinazogharimu uhai wa watu wengi. Sheria yetu inayo mapungufu kadhaa pamoja na juhudi nyingi za Jeshi la Polisi na wadau wengine kutaka kudhibiti jambo hili limeendelea kuwa tatizo. Adhabu zisizokidhi wala kuleta hofu kwa maderava wasiotaka kutii zimeendelea kufifisha juhudi za kudhibiti tatizo hili.

 Tunatoa wito kwa watunga sera kushirikiana zaidi na wadau kuuelimisha umma katika eneo la uhusiano wa adhabu zitokanazo na makosa ya usalama barabarani na ongezeko la ajali. Pia sheria kufanyiwa maboresho na kuangalia kwa upya mianya iliyopo.

TAMKO HILI LIMETOLEWA LEO NA MTANDAO WA WADAU KUTOKA ASASI ZA KIRAIA:

 1. TAWLA
 2. TAMWA
 3. WLAC
 4. TCRF
 5. TLS
 6. TMF
 7. RSA
 8. AMEND TANZANIA
 9. SHIVYAWATA
 10. TABOA &
 11. SAFE SPEED FOUNDATION

 

MTANDAO WA WADAU KUTOKA ASASI ZA KIRAIA UNAOTETEA MAREKEBISHO YA SHERIA NA SERA INAYOHUSU USALAMA BARABARANI TANZANIA

CHAMA Cha waandishi wa habari Tanzania (TAMWA) leo  imekutana na wahariri wa vyombo vya habari nchini ili kuwaeleza kuhusu programu mpya ya miaka mitano katika Masuala ya utawala bora na haki inayodhaminiwa na Shirika la maendeleo la Denmark (DANIDA)

 Lengo la programu hiyo ni  kuchangia katika uboreshaji wa hali ya maisha ya wanawake na wanaume kupitia msaada ambao utakuza usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake, demokrasia, utawala bora na kuheshimu haki za binadamu nchini Tanzania.

 Wahariri wamekiri kuwepo kwa changamoto katika kuandika habari za ukatili wa kijinsia nchini ikiwemo ukosefu wa takimu sahihi na mazingira magumu ya kuandika habari hizo.

TAMWA YAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI

Mkurugenzi wa Idara ya Umma (Public Affairs Officer) na Msemaji wa Ubalozi USAID, Bi Marissa Mauver, alitembelea Ofisi za Jumanne 13/06/2017 na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bibi Edda Sanga. Bi Marissa Mauver, ameisifu TAMWA kwa kazi nzuri inayofanya kutetea haki za wannawake na watoto na kusema kwamba kazi hiyo ni muhimu katika ujenzi wa jamii inayojali utawala bora na haki za binadamu.

MKURUGENZI WA IDARA YA UMMA (Public Affairs Officer) NA MSEMAJI WA UBALOZI WA USAID AITEMBELEA TAMWA

Siku ya mtoto wa Afrika huazimishwa tarehe 16/06 kila mwaka. Siku hii ilianzishwa na OAU (organization of Africa Unit) na imeanza kuazimishwa toka mwaka 1991 ili kuwapa heshima watoto wale ambao walishiriki maandamano ya Soweto mwaka 1976.

Katika maandamano haya ya Soweto, zaidi ya watoto 10,000 walioshirikiki maandamano kati yao waliuwawa na wengine walijeruhiwa. Haya yaliwakuta wakiwa katika harakati za kutetea haki zao, miongoni mwa hayo ni elimu bora na yenye kukidhi matakwa yao.

Siku hii ya mtoto wa Africa ambayo kauli mbiu yake kitaifa ni “Maendeleo endelevu 2030: Imarisha ulinzi na Fursa sawa kwa watoto” ambayo inalenga jamii kuwajibika ipasavyo kwa watoto, kwetu TAMWA na wadau wengine washiriki, inatukutanisha na ninyi waandishi wa habari kujadili changamoto zinazowakabili watoto wa Taifa letu la Kitanzania sasa na siku za usoni. Miongoni mwa changamoto hizo ni ukatili wa kijinsia katika ngazi ya  familia. Tukumbuke kwamba familia ni taasisi inayojitegemea na yenye utaratibu, kanuni na uongozi kamili. Malezi na makuzi ndiyo dira, maono na dhamira yetu kwa watoto wetu.

Katika malezi tunatazamia matendo yote yafanywe na wazazi/walezi na jamii, kwa lengo la kumlea, kumkuza kumlinda, na kumwendeleza mtoto kimwili, kikakili, kihisia na kimaadili ili aweze  kukua vizuri na kukabiliana na changamoto za kijamii.

Ni dhahiri kwamba misingi hii bora ya malezi na makuzi kwa watoto wetu imeporomoka kabisa. Hali hii imepelekea watoto katika jamii zetu kufanyiwa ukatili wa kiwango cha juu kabisa.  Familia zetu siyo salama tena.  Tumepoteza utu na misingi mizuri ya imani ya dini, mila na desturi nzuri za mtanzania. Kiwango cha ukatili wa watoto majumbani kimepanda hadi kufikia asilimia 49 mwaka 2017.  Kiwango hiki ni cha juu zaidi ya kile cha asilimia 15% cha watoto kufanyiwa ukatili shuleni na asilimia 23% cha watoto kufanyiwa ukatili sehemu nyingine.

Kwa uhalisia huu, ukatili wa majumbani hauwezi kutuacha salama kama hatutachukua hatua kama wazazi/walezi ndugu na jamaa. Ukatili  wa kijinsia kwa watoto wa kike na kiume umeenea sana kwenye jamii nyingi Tanzania.

Tafiti zinaonyesha kuwa watendaji wa ukatili huu ni watu wa karibu sana na wengine huwa ni waathirika wa vitendo hivyo wakiwemo wazazi, welezi, ndugu jamaa, na majirani au waajiri. Sababu kubwa za ukatili huu ni pamoja na mitazamo ya kijamii kuhusu ukatili na unyanyasaji, uwezo wa mifumo ya ulinzi na ustawi wa jamii.

 

Tukumbuke ukatili wa jinsia utaligharimu Taifa na jamii kwa kiwango cha  juu kwa sasa na baadae. Ukatili dhidi ya watoto una madhara makubwa kwa afya ya mtoto kihisia, kitabia na kimwili. Pia huathiri maendeleo ya mtoto kijamii katika maisha yake yote. Watoto wanaotendewa ukatili, unyanyasaji na unyonyaji hukabiliwa na hatari ya kufanya vibaya katika masomo yao. Aidha vitendo vya kikatili ndio sababu kubwa ya watoto kukimbia nyumbani na kwenda kuishi mitaani. Hii huongeza uwezekano wa watoto kuishi katika mazingira ya umaskini. Pia upo mwanya kwa watoto kuendeleza vitendo vya ukatili kwa watoto/wenzao na si hivyo tu pia wanapokuwa watu wazima huuendeleza ukatili huo kwa watoto wao na kujihusisha na tabia nyingine zisizokubalika kijamii na ambazo huigharimu jamii.

Watoto waliowahi kufanyiwa ukatili wapo katika uwezekano mkubwa wa kujiingiza katika tabia hatarishi ambazo huweza kuwasababishia hata maambukizo ya VVU/UKIMWI,  matumizi ya dawa za kuleya, wizi, ujambazi na hata ugaidi.

Utafiti wa ukatili mwaka 2015/16 kwa watoto umegundua kuwa watoto wa kike na wakiume wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia kwa sasa , wana uwezekano mkubwa zaidi wa kufanya ngono na wapenzi wengi kuliko wale ambao hawafanyiwi ukatili. Hali hii inaibuwa wasiwasi wa  ongezeko la maambukizi ya VVU kwa kundi hili. Kundi hili lipo katika hatari ya kufanya biashara ya ngono ili kupata fedha au vitu vingine.

Viwango vya ukatili unaohusisha ngono vinaongezeka kulingana na umri, kuanzia asilimia 8 kwa wanawake wenye umri wa miaka 15-19 hadi asilimia 18 kwa wanawake wenye umri wa miaka 40 – 49. Aidha wanawake 4 kati ya 10 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15 nchini Tanzania, kama ambavyo vimebainishwa na Utafiti wa Ukatili dhidi ya Watoto na Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya Tanzania mwaka 2015 /16.

Katika hali isiyoweza kuelezeka hivi karibuni Wanafunzi 101 wamepewa ujauzito katika kipindi cha miezi sita kwa mwaka huu 2017, matukio hayo yametokea Mkoani mwanza wilayani ukerewe. Kwa masikitiko makubwa inasemekana vitendo hivyo vimefanywa na viongozi ngazi ya kata na vijiji. Na imethibitika kuwa wazazi na serekali za vijiji ndiyo kichocheo kikubwa kwa watoto  kupata ujauzito(Tanzania Daima 12/6/2017) Je ni watoto wangapi walifanyiwa ukatili huo na hawakupata mimba?Je ni wavulana wangapi walifanyiwa ukatili huo?

Tanzania ipo katika hatari kubwa sana ya kuwa nchi yenye watoto na vijana (Waliopo katika kundi hatarishi (Key Population) ifikapo 2030 endapo jitihada za lazima juu ya ulinzi, malezi na makuzi bora, ya watoto wetu hayatazingatiwa. Ukatili dhidi ya watoto wetu unaosababishwa/kufanywa na wazazi na walezi majumbani ni mkubwa katika jamii zetu ambapo wakati mwingine mama amediriki kumchoma mtoto wake kwa kosa la kuiba kiasi cha shilling 7000 (Mtanzania 12/6/2017).

Ndoto za watoto wetu zimezimwa ghafula. Ukatili dhidi ya  watoto  wetu kamwe hautatuacha salama. Kwa mfano mkoani Katavi mtoto wa kike alibakwa hadi kupoteza maisha(Majira 12/6/2017).Huu ni Unyama usiokuwa na mfano. Veronika Lucas(13) ndoto zake zakuwa rubani zimezikwa. Siku moja kabla ya mauti alimjulisha mama yake ndoto zake za kuwa rubani wa Tanzania,lakini ukatili wa kinyama ulizika matumaini yake. Tunakusihi ewe Yarabi umpekee veronica lucas kama ulivyompokea Yabili

Wazazi tumekosa utu. Sisi ndiyo wachochezi na watekelezaji wa ukatili dhidi ya watoto. Malezi yetu na makuzi yamekuwa na ukatili usio kifani. Tumeyasahau majukumu na wajibu wetu kama wazazi/ walezi. Malezi na makuzi siyo salama kwa watoto wetu, makundi rika na mitandao isiyokuwa na maadili imechukua sehemu yetu wazazi. Kizazi kijacho hakina matumaini,kimetelekezwa.

Kupitia kwenu waandishi wa habari, tunatoa wito kwa umma wa watazania wazazi na walezi, kuwa milango yetu TAMWA ipo wazi kukusaidia wewe mzazi/ mlezi kulea vyema. Ni imani yetu kuwa UKIMPENDA MTOTO UTAMLINDA

 

Malengo Mahsusi

 1. Kutoa mwongozo kwa waaandishi wa habari wawezeshaji wengine wa jamii katika ngazi ya jamii kuhusu stadi za malezi kuzuia Ukatili Dhidi ya Watoto
 2. Kuongeza uelewa na kuhamasisha uzingatiaji wa stadi zisizo katili katika malezi na makuzi ya watoto miongoni mwa wazazi na walezi wengine.
 3. Kuogeza uwezo wa wazazi na walezi, kuzungumza kwa uwazi kuhusu ukatili unaondelea katika jamii; na hivyo kutoa jukwaa la majadiliano kuhusu ukatili dhidi ya watoto kama fursa kwa jamii kukiri na kutambua yale yasiyokubalika na kujadiliana utaratibu wa kuyazuia.
SIKU YA MTOTO WA AFRICA 16/6/2017

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), leo Tarehe 9 August, 2017 kimewakutanisha wafanyakazi wake kutoka Tanzania Bara na Zanzibar katika mkutano wa siku 3 unaofanyika katika hoteli ya Mbezi Garden jijini Dare s salaam.  Lengo kuu ni kushiriki pamoja katika kupitia na kuboresha mfumo wa ufatiliaji na tathmini ya programu yake mpya inayohusu utawala na haki za binadamu inayofadhiliwa na mfuko wa maendeleo wa DANIDA. Mradi huo unalenga kuwakinga wanawake na watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia na kuweka mfumo bora wa taarifa zinazohusu ukatili huo ili jamii ichukue hatua kuhakikisha sheria inafuata mkondo wake.

Mradi huo unatekelezwa katika wilaya 10 za Tanzania Bara na Zanzibar ambazo ni  Ilala, Kinondoni, Kisarawe, Mvomero, Ruangwa, Lindi Vijijini, Newala, Mjini Magharibi, Kusini Unguja and Wete Pemba. TAMWA inaamini kuwa vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika mabadiliko ya jamii yanayoweza kusaidia kuleta maendeleo na ustawi wa Taifa.

TAMWA YAKUTANISHA WAFANYAKAZI WAKE TANZANIA BARA NA ZANZIBAR KUBORESHA MFUMO WA UFUATILIAJI NA TATHMINI WA MRADI WAKE MPYA

WELCOME TO TAMWA WEBSITE

 The Tanzania Media Women’s Association (TAMWA) is a non-profit sharing, non-governmental and non-partisan organisation registered under the Societies Ordinance on 17th of November 1987 with registration number SO 6763. The Association

Contemporary educational background approach does its best to engulf classmates in exploring concept, providing them with quite a few tasks to figure on as it may. Prerequisites for some types of educational paperwork boost routine buy essay Who knew essay article writing could well be so really difficult. To tell the truth, at basic tier, it has been hardly ever quite hard, but like we rise the academic concentrations it can get harder and tougher

in 2004 complied with the new NGO law of 2002. Tamwa has two offices in Dar -es- Salaam and Zanzibar. Zanzibar office located at Mombasa area near SOS is rented, but the office in Dar -es-Salaam situated at Sinza-Mori,  along Shekilango Road, Kijitonyama, Kinondoni District, is Association's property.

The founder members of TAMWA are; Fatma Alloo, Edda Sanga, Leila Sheikh, Rose Haji, Ananilea Nkya, Valerie Msoka, Pili Mtambalike, Elizabeth Marealle, Rose Kalemera,  Jamilla Chipo, Nellie Kidela and Halima Shariff.  Currently the Association has over 100 members with a minimum qualification of Diploma in Journalism and three years work experience in the media industry. Members are working in public and private media houses as editors, reporters, programme managers, producers, public relations and communication officers. The AGM is the supreme organ of the Association but it delegates its powers our to the GB which meets four times a year to evaluate the performance  of the Secretariat an organ to execute day today activities of the Association.

OUR YOUTUBE VIDEOS

Visitors Counter

1310401
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
78
2284
10134
1277669
55518
76064
1310401

Your IP: 54.80.113.185
2017-08-24 01:01

Events - Calendar

August 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31

FOLLOW US ON FACEBOOK

Map

JoomShaper