NEW MARCH 27,2015

11 April 2015 Written by 
Published in News
March 27,2015 Zaidi ya Wanachama 100 wa Chama cha Wanahabari Wanawake nchini- TAMWA Jumamosi tarehe 28th Machi, 2015 wanafanya Mkutano wake Mkuu wa mwaka 2014 ambapo pamoja na mambo mengine wanachama watapata fursa ya  kutathmini kazi zilizofanyika  mwaka 2014, na utekelezaji wa mpango mkakati wa 2015-2021. Mkutano huo utaanza saa 2:00 asubuhi katika ofisi za chama zilizoko Sinza Mori, Dar es Salaam.
  Mkutano huo ulianza na mafunzo Ijumaa tarehe 27th Machi mwaka huu na kuwapa fursa wanachama kujadili mafanikio yaliyopatikana kwenye mpango mkakati wa miaka mitano iliyopita (2009 -2014) pamoja na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji ambapo pia watamchagua Mwenyekiti mpya baada ya aliyekuwepo kumaliza muda wake. Aidha baada ya mkutano huo wanachama watajumuika pamoja katika hafla ya kuchangia mfuko wa shughuli za TAMWA (Gala Dinner) ambazo ni pamoja na kupiga vita vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto itakayofanyika jioni katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Mkutano mkuu wa TAMWA ndicho chombo cha juu chenye mamlaka ya kurekebisha katiba yake, kuingiza wanachama wapya, kuchagua viongozi, kupitisha ripoti za mwaka na kutoa maamuzi kuhusu mipango na mikakati ya chama kuhusu utetezi.          
Rate this item
(0 votes)

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

August 2016
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper