×

Error

Error 403 - Forbidden (no access permissions) for http://www.tamwa.org/modules/mod_latestnewsenhanced/animationmaster.js.php

Error 403 - Forbidden (no access permissions) for http://www.tamwa.org/modules/mod_latestnewsenhanced/stylemaster.css.php

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAMWA KUTAMBULISHA KWENYE KATA MRADI WA UNYWAJI POMBE KUPINDUKIA

23 August 2015 Written by 
Published in PRESS RELEASE
  Chama cha Wanahabari Wanawake - TAMWA leo, tarehe 24 Agost, 2015 katika ofisi zake, Sinza Mori kinakutana na viongozi wa mitaa, wadau na vikundi vya jamii, Kata za Saranga na Wazo Hill, kutambulisha mradi wenye lengo la kutokomeza ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji pombe kupindukia wa IOGT.
Mradi huo unaotekelezwa katika kata tatu za Wilaya ya kinondoni, Dar es Salaam ambazo ni Makumbusho, Saranga na Wazo Hill, unalengo la kutekeleza mikakati ya kuhakikisha zinawekwa sera na sheria zitakazosaidia katika kupunguza ukatili wa kijinsia unaotokana  na matumizi ya unywaji pombe kupindukia. Aidha mradi umekuja kipindi ambacho ukatili wa kijinsia hasa ule unaofanywa na wanaume kuwatelekeza wanawake na familia zao pamoja na ubakaji unaofanywa na ndugu wa karibu kufanyika kila mara, vitendo ambavyo vimekuwa vikiongezeka kutokana na ulevi wa pombe. TAMWA imekuwa ikipata kesi za ukatili kupitia kituo chake cha Usuluhishi-CRC na kubaini kuwa vitendo vya wanawake kutelekezwa vimeongezeka, ambapo kwa kipindi cha miezi sita ya Juni hadi Desemba mwaka 2014 kilipokea kesi 34 ziliongezeka na kufikia kesi 53 kwa miezi sita ya mwaka 2015 kuanzia Januari hadi Juni. TAMWA inaamini kuwa, kama wanaume watatambua majukumu na umuhimu wao na kuachana na unywaji pombe kupindukia unaosababisha vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na  ubakaji, wanawake na watoto kutelekezwa, vipigo kwa wanawake, watoto kulazimishwa kuolewa, maisha ya familia yataboreshwa pamoja na maendeleo ya jamii, kiuchumi na Taifa kwa ujumla.   Edda Sanga Mkurugenzi Mtendaji       PRESS RELEASE   TAMWA TO INTRODUCE ALCOHOLISM PROJECT IN WARDS                                                             Tanzania Media Women’s Association – TAMWA today on 24th August, 2015 at its offices, Sinza Mori, Dar es Salaam will meet with local leaders, stakeholders and community groups from Saranga and Wazo Hill Ward to introduce the IOGT project aimed at combating excessive alcohol that contribute to Gender Based Violence (GBV).   The project being implemented in three wards of Kinondoni, Dar es Salaam at  Makumbusho, Saranga and Wazo Hill, intended to set strategies ensuring that policies and laws support the efforts to combat the alcoholism that contribute to gender based violence.   Additionally; the project has come at a right time when gender based violence especially those perpetrated by the excessive consumption of alcohol such as abandonment of women and children and rape are on the increase.   TAMWA has been receiving cases of violence through its Crisis Resolving Centre-CRC and realized the increase of acts of abandonment of women, whereas for the period of six-month from June to December, 2014 received 34 cases increased to 53 cases in the six months of January to June, 2015.   TAMWA believes that, through its interventions, men will take responsibilities to stop the excessive alcohol consumption which contribute to gender based violence and ultimately improve the wellbeing of the families and promote development in communities and the nation at large.     Edda Sanga Executive Director
Read 239775 times Last modified on Thursday, 27 August 2015 13:12
Rate this item
(0 votes)

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

July 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper