×

Error

Error 403 - Forbidden (no access permissions) for http://www.tamwa.org/modules/mod_latestnewsenhanced/animationmaster.js.php

Error 403 - Forbidden (no access permissions) for http://www.tamwa.org/modules/mod_latestnewsenhanced/stylemaster.css.php

KUPINGA NDOA ZA UTOTONI :FEBRUARY 24,2015

12 April 2015 Written by 
Published in PRESS RELEASE
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI UBALOZI WA KANADA KUMTUNUKU MKURUGENZI MTENDAJI WA TAMWA KUWA BALOZI WA KUPINGA NDOA ZA UTOTONI Ubalozi wa Canada nchini Tanzania kwa mara ya kwanza utamkabidhi Muurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Valerie Msoka kuwa balozi wa kampeni ya kupinga ndoa za utotoni (CEFM). Kwa mujibu wa Ubalozi huo, tukio hilo litafanyika leo, Februari 24, 2015 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8 mchana. Hafla hiyo itahudhuriwa, miongoni mwa watu wengine, na Katibu Mkuu Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Anna Maembe, Balozi wa Canada nchini Tanzania, Alexandre Lévêque, Msaidizi wa Balozi wa Canada anayehusika na masuala ya kisiasa, Eric Bertram, na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na vyombo vya habari.
  CEFM inatambua mchango uliotolewa na mtu ambaye ametumia jitihada na muda wake mwingi katika kutetea haki za watoto na ambaye amekuwa akiunga mkono harakati za kuhakikisha taifa letu linakua mahali salama kwa watoto hasa watoto wa kike katika kizazi cha sasa na kijacho. Kutokana na uzoefu wake wa kupigania haki za biandamu hasa haki za wanawake na watoto, Valerie, ameifanya TAMWA kuwa jina la kukumbukwa katika kuleta usawa na haki za wanawake na watoto. Majukumu yake ya hivi karibuni ni pamoja na: Mbunge katika Bunge Maalum la Katiba: Alifikisha masuala ya ndoa za utotoni nchini Tanzania katika bunge hilo na haja ya kuingiza umri wa motto unaotambulika kisheria katika katiba. Hii ilisababisha kamati za Bunge hilo kupendekeza umri wa motto kikatiba kuanzia 0 hadi miaka 18. Mjumbe wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba: Aliweza kutetea masuala ya usawa ndani ya kamati ikiwa ni pamoja na haki ya kumlinda mtoto wa kike na wanawake dhidi yya mila potofu ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni, ukeketaji, haki ya kumiliki ardhi na uongozi. Mjumbe wa Mtandao wa Kupinga Ndoa za Utotoni Tanzania (TECMN): Aliwezesha kuundwa kwa ukanda huru wa kukomesha ndoa za utotoni nchini Tanzania (Agosti 2014) kwa kuwa mwezeshaji wa tukio hilo jijini Dar es salaam mbele ya rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, mgeni rasmi Graca Machel, wakuu wa Balozi mbalimbali nchini na mashirika ya Umoja wa Mataifa. Kutambuliwa kwake kuwa Balozi wa Kampeni ya Kupinga Ndoa za Utotoni, kutaleta hamasa zaidi na kumfanya kuongeza jitihada, nguvu na kutoa muda wake zaidi katika kutetea haki za watoto nchini Tanzania. Valerie N. Msoka Mkurugenzi Mtendaji  
Read 123130 times Last modified on Sunday, 12 April 2015 08:39
Rate this item
(0 votes)

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

August 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper