FLAT YENYE VYUMBA VIWILI, SEBULE, MALIWATO NA JIKO INAPANGISHWA KWA BEI NAFUU. IPO KISUTU SOKONI. MAWASILIANO PIGA: 0222772681 AU 0222771005 AU 0754285701

FLAT INAPANGISHWA

Mkurugenzi wa Idara ya Umma (Public Affairs Officer) na Msemaji wa Ubalozi USAID, Bi Marissa Mauver, alitembelea Ofisi za Jumanne 13/06/2017 na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bibi Edda Sanga. Bi Marissa Mauver, ameisifu TAMWA kwa kazi nzuri inayofanya kutetea haki za wannawake na watoto na kusema kwamba kazi hiyo ni muhimu katika ujenzi wa jamii inayojali utawala bora na haki za binadamu.

MKURUGENZI WA IDARA YA UMMA (Public Affairs Officer) NA MSEMAJI WA UBALOZI WA USAID AITEMBELEA TAMWA

Siku ya mtoto wa Afrika huazimishwa tarehe 16/06 kila mwaka. Siku hii ilianzishwa na OAU (organization of Africa Unit) na imeanza kuazimishwa toka mwaka 1991 ili kuwapa heshima watoto wale ambao walishiriki maandamano ya Soweto mwaka 1976.

Katika maandamano haya ya Soweto, zaidi ya watoto 10,000 walioshirikiki maandamano kati yao waliuwawa na wengine walijeruhiwa. Haya yaliwakuta wakiwa katika harakati za kutetea haki zao, miongoni mwa hayo ni elimu bora na yenye kukidhi matakwa yao.

Siku hii ya mtoto wa Africa ambayo kauli mbiu yake kitaifa ni “Maendeleo endelevu 2030: Imarisha ulinzi na Fursa sawa kwa watoto” ambayo inalenga jamii kuwajibika ipasavyo kwa watoto, kwetu TAMWA na wadau wengine washiriki, inatukutanisha na ninyi waandishi wa habari kujadili changamoto zinazowakabili watoto wa Taifa letu la Kitanzania sasa na siku za usoni. Miongoni mwa changamoto hizo ni ukatili wa kijinsia katika ngazi ya  familia. Tukumbuke kwamba familia ni taasisi inayojitegemea na yenye utaratibu, kanuni na uongozi kamili. Malezi na makuzi ndiyo dira, maono na dhamira yetu kwa watoto wetu.

Katika malezi tunatazamia matendo yote yafanywe na wazazi/walezi na jamii, kwa lengo la kumlea, kumkuza kumlinda, na kumwendeleza mtoto kimwili, kikakili, kihisia na kimaadili ili aweze  kukua vizuri na kukabiliana na changamoto za kijamii.

Ni dhahiri kwamba misingi hii bora ya malezi na makuzi kwa watoto wetu imeporomoka kabisa. Hali hii imepelekea watoto katika jamii zetu kufanyiwa ukatili wa kiwango cha juu kabisa.  Familia zetu siyo salama tena.  Tumepoteza utu na misingi mizuri ya imani ya dini, mila na desturi nzuri za mtanzania. Kiwango cha ukatili wa watoto majumbani kimepanda hadi kufikia asilimia 49 mwaka 2017.  Kiwango hiki ni cha juu zaidi ya kile cha asilimia 15% cha watoto kufanyiwa ukatili shuleni na asilimia 23% cha watoto kufanyiwa ukatili sehemu nyingine.

Kwa uhalisia huu, ukatili wa majumbani hauwezi kutuacha salama kama hatutachukua hatua kama wazazi/walezi ndugu na jamaa. Ukatili  wa kijinsia kwa watoto wa kike na kiume umeenea sana kwenye jamii nyingi Tanzania.

Tafiti zinaonyesha kuwa watendaji wa ukatili huu ni watu wa karibu sana na wengine huwa ni waathirika wa vitendo hivyo wakiwemo wazazi, welezi, ndugu jamaa, na majirani au waajiri. Sababu kubwa za ukatili huu ni pamoja na mitazamo ya kijamii kuhusu ukatili na unyanyasaji, uwezo wa mifumo ya ulinzi na ustawi wa jamii.

 

Tukumbuke ukatili wa jinsia utaligharimu Taifa na jamii kwa kiwango cha  juu kwa sasa na baadae. Ukatili dhidi ya watoto una madhara makubwa kwa afya ya mtoto kihisia, kitabia na kimwili. Pia huathiri maendeleo ya mtoto kijamii katika maisha yake yote. Watoto wanaotendewa ukatili, unyanyasaji na unyonyaji hukabiliwa na hatari ya kufanya vibaya katika masomo yao. Aidha vitendo vya kikatili ndio sababu kubwa ya watoto kukimbia nyumbani na kwenda kuishi mitaani. Hii huongeza uwezekano wa watoto kuishi katika mazingira ya umaskini. Pia upo mwanya kwa watoto kuendeleza vitendo vya ukatili kwa watoto/wenzao na si hivyo tu pia wanapokuwa watu wazima huuendeleza ukatili huo kwa watoto wao na kujihusisha na tabia nyingine zisizokubalika kijamii na ambazo huigharimu jamii.

Watoto waliowahi kufanyiwa ukatili wapo katika uwezekano mkubwa wa kujiingiza katika tabia hatarishi ambazo huweza kuwasababishia hata maambukizo ya VVU/UKIMWI,  matumizi ya dawa za kuleya, wizi, ujambazi na hata ugaidi.

Utafiti wa ukatili mwaka 2015/16 kwa watoto umegundua kuwa watoto wa kike na wakiume wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia kwa sasa , wana uwezekano mkubwa zaidi wa kufanya ngono na wapenzi wengi kuliko wale ambao hawafanyiwi ukatili. Hali hii inaibuwa wasiwasi wa  ongezeko la maambukizi ya VVU kwa kundi hili. Kundi hili lipo katika hatari ya kufanya biashara ya ngono ili kupata fedha au vitu vingine.

Viwango vya ukatili unaohusisha ngono vinaongezeka kulingana na umri, kuanzia asilimia 8 kwa wanawake wenye umri wa miaka 15-19 hadi asilimia 18 kwa wanawake wenye umri wa miaka 40 – 49. Aidha wanawake 4 kati ya 10 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15 nchini Tanzania, kama ambavyo vimebainishwa na Utafiti wa Ukatili dhidi ya Watoto na Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya Tanzania mwaka 2015 /16.

Katika hali isiyoweza kuelezeka hivi karibuni Wanafunzi 101 wamepewa ujauzito katika kipindi cha miezi sita kwa mwaka huu 2017, matukio hayo yametokea Mkoani mwanza wilayani ukerewe. Kwa masikitiko makubwa inasemekana vitendo hivyo vimefanywa na viongozi ngazi ya kata na vijiji. Na imethibitika kuwa wazazi na serekali za vijiji ndiyo kichocheo kikubwa kwa watoto  kupata ujauzito(Tanzania Daima 12/6/2017) Je ni watoto wangapi walifanyiwa ukatili huo na hawakupata mimba?Je ni wavulana wangapi walifanyiwa ukatili huo?

Tanzania ipo katika hatari kubwa sana ya kuwa nchi yenye watoto na vijana (Waliopo katika kundi hatarishi (Key Population) ifikapo 2030 endapo jitihada za lazima juu ya ulinzi, malezi na makuzi bora, ya watoto wetu hayatazingatiwa. Ukatili dhidi ya watoto wetu unaosababishwa/kufanywa na wazazi na walezi majumbani ni mkubwa katika jamii zetu ambapo wakati mwingine mama amediriki kumchoma mtoto wake kwa kosa la kuiba kiasi cha shilling 7000 (Mtanzania 12/6/2017).

Ndoto za watoto wetu zimezimwa ghafula. Ukatili dhidi ya  watoto  wetu kamwe hautatuacha salama. Kwa mfano mkoani Katavi mtoto wa kike alibakwa hadi kupoteza maisha(Majira 12/6/2017).Huu ni Unyama usiokuwa na mfano. Veronika Lucas(13) ndoto zake zakuwa rubani zimezikwa. Siku moja kabla ya mauti alimjulisha mama yake ndoto zake za kuwa rubani wa Tanzania,lakini ukatili wa kinyama ulizika matumaini yake. Tunakusihi ewe Yarabi umpekee veronica lucas kama ulivyompokea Yabili

Wazazi tumekosa utu. Sisi ndiyo wachochezi na watekelezaji wa ukatili dhidi ya watoto. Malezi yetu na makuzi yamekuwa na ukatili usio kifani. Tumeyasahau majukumu na wajibu wetu kama wazazi/ walezi. Malezi na makuzi siyo salama kwa watoto wetu, makundi rika na mitandao isiyokuwa na maadili imechukua sehemu yetu wazazi. Kizazi kijacho hakina matumaini,kimetelekezwa.

Kupitia kwenu waandishi wa habari, tunatoa wito kwa umma wa watazania wazazi na walezi, kuwa milango yetu TAMWA ipo wazi kukusaidia wewe mzazi/ mlezi kulea vyema. Ni imani yetu kuwa UKIMPENDA MTOTO UTAMLINDA

 

Malengo Mahsusi

  1. Kutoa mwongozo kwa waaandishi wa habari wawezeshaji wengine wa jamii katika ngazi ya jamii kuhusu stadi za malezi kuzuia Ukatili Dhidi ya Watoto
  2. Kuongeza uelewa na kuhamasisha uzingatiaji wa stadi zisizo katili katika malezi na makuzi ya watoto miongoni mwa wazazi na walezi wengine.
  3. Kuogeza uwezo wa wazazi na walezi, kuzungumza kwa uwazi kuhusu ukatili unaondelea katika jamii; na hivyo kutoa jukwaa la majadiliano kuhusu ukatili dhidi ya watoto kama fursa kwa jamii kukiri na kutambua yale yasiyokubalika na kujadiliana utaratibu wa kuyazuia.
SIKU YA MTOTO WA AFRICA 16/6/2017

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), leo Tarehe 9 August, 2017 kimewakutanisha wafanyakazi wake kutoka Tanzania Bara na Zanzibar katika mkutano wa siku 3 unaofanyika katika hoteli ya Mbezi Garden jijini Dare s salaam.  Lengo kuu ni kushiriki pamoja katika kupitia na kuboresha mfumo wa ufatiliaji na tathmini ya programu yake mpya inayohusu utawala na haki za binadamu inayofadhiliwa na mfuko wa maendeleo wa DANIDA. Mradi huo unalenga kuwakinga wanawake na watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia na kuweka mfumo bora wa taarifa zinazohusu ukatili huo ili jamii ichukue hatua kuhakikisha sheria inafuata mkondo wake.

Mradi huo unatekelezwa katika wilaya 10 za Tanzania Bara na Zanzibar ambazo ni  Ilala, Kinondoni, Kisarawe, Mvomero, Ruangwa, Lindi Vijijini, Newala, Mjini Magharibi, Kusini Unguja and Wete Pemba. TAMWA inaamini kuwa vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika mabadiliko ya jamii yanayoweza kusaidia kuleta maendeleo na ustawi wa Taifa.

TAMWA YAKUTANISHA WAFANYAKAZI WAKE TANZANIA BARA NA ZANZIBAR KUBORESHA MFUMO WA UFUATILIAJI NA TATHMINI WA MRADI WAKE MPYA

Wanaharakati wenzangu, karibuni TAMWA, mahali adhimu ambapo tumeamua kuzindulia maadhimisho ya miaka 30 ya Chama Cha Wandishi Wa Habari Wanawake Tanzania. Jina la TAMWA si geni masikioni mwa Watanzania walio wengi, ikizingatiwa hiki ni chama kikongwe cha wanahabari Tanzania ambacho mithili ya chombo baharini, kimehimili mawimbi, makubwa na madogo, mitikisiko na misukosuko ya hapa na pale, na bado kikaweza kuelea katika bahari tulivu. Itoshe kusema, tumetoka mbali. Mimi mbele yenu ni mmoja wa waasisi wa Chama Cha TAMWA, kwa niaba ya wenzangu kumi na mmoja, tulio hai ni kumi, ambapo wawili wametangulia mbele za haki. Namshukuru Mungu ametujalia neema ya kuuona Mwaka uliotutunuku fursa ya kuanzisha Chama hiki, japokuwa tunazindua harakati za maadhimisho haya, tukiwa na takriban siku 78 kufikia kilele hapo tarehe 17 Novemba Mwaka huu.

Tungependa ndugu zetu, marafiki zetu, wadau wetu, Watanzania wenzetu mmoja mmoja na katika ujumla wenu, muungane nasi kufurahia fursa hii ya kuadhimisha siku hii muhimu ambayo katika historia ya kuwepo kwetu, tunahesabu mafanikio lukuki tuliyoyapata.

Moja ya mafanikio hayo ambayo ni vigumu kusahau ni ushawishi, kuzengea na kuzonga kuliko fanyika kwa ustadi mkubwa , tukiwa na wenzetu TGNP, TAWLA, MEWATA, WLAC, LHRC, CRC na mashirika mengine kama hamsini hivi tukitetea kubadilika kwa sera, na sheria kandamizi zinazomnyima haki mwanamke na mtoto, hasa mtoto wa kike. Furaha yetu ilikamilika , pale Mwaka 1998 tulipofanikiwa kuongea na wabunge, wakatuelewa na kuwazawadia Watanzania SHERIA YA MAKOSA YA KUJAMIIANA , maarufu kama SOSPA. Utakumbuka pia sheria hii iliboreshwa Mwaka 2005

Uzuri wa sheria hii ya SOSPA, ni kwamba kwa mara ya kwanza, ilitamkwa wazi kuwa ukeketaji ni kosa la jinai, ikampa mtoto wa kike ulinzi wa kutofanyiwa ukatili akiwa chini ya umri wa miaka 18. Huko Zanzibar, sheria ya spinster ambayo ilimtaka mtoto wa kike aliyepata mimba chini ya umri wa miaka 18 afukuzwe shule na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela, wakati mwanaume aliachwa huru kutokana na kutokuwa na kifaa cha DNA, marekebisho yalifanyika katika sheria hiyo ambapo kifungo kwa mtoto wa kike kilifutwa na mwanamume aliyempa mimba anawajibika kutoa matunzo ya mtoto hadi atakapofika miaka 18.

Januari 2008 ulizinduliwa mpango wa kuboresha hali za wanawake kiuchumi na kijamii uitwao WEZA, ambao ulitekelezwa na shirika la CARE TANZANIA, kwa kushirikiana na TAMWA ZBR. Mpango huu uliangalia shehia ya Unguja Kusini, na Kaskazini Pemba kwa kuhusisha makundi 300 ya wanawake 6,000 ambao waliunda vikundi vya kuweka na kukopeshana kwa ajili ya uwekezaji katika miradi ya uzalishaji mali na kuongeza kipato kwa ajili ya ustawi wa jamii. Azma hii ni katika kuhalalisha usemi maarufu kwamba ukimwezesha mwanamke, umeiwezesha jamii.

Mafanikio zaidi ni pale kwa kushirikiana na wenzetu wanasheria, Mwaka 1999 sheria ya ardhi na sheria ya ardhi ya vijiji, iltoa fursa kwa wanawake kumiliki ardhi, na kwa mara ya kwanza, wanawake waliruhusiwa kushiriki katika kutoa suluhu ya migogoro ya ardhi.

TAMWA, kwa ujasiri mkubwa, ilivunja ukimya wa mauaji ya vikongwe yaliyokuwa yakiendelea Shinyanga na kufanikiwa kufanya suala hilo liwe ajenda ya kitaifa. Aidha kwa kutumia vyombo vya habari tukishirikiana na mashirika mengine, tulifanikiwa kuongeza idadi ya wanawake bungeni kutoka asili mia 20 mwaka 2000 hadi 36 mwaka 2005 na kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, tulimpata spika wa bunge mwanamke, Mama ANNE Semamba Makinda ambaye ametuwakilisha vizuri hadi alipostaafu.

Kama kuna kazi kubwa na ya kusifika imefanywa, na inaendelea kufanywa kwa ufadhili wa DANIDA toka mwaka 2012 ni katika GBV, ambapo TAMWA ikishiriana na CRC kituo cha usuluhishi na ushauri nasihi , na bila kusahau bang style ambayo kwa mfumo wake inafanana na kampeni. Mfumo huu tuliutumia sana TAMWA, ambapo vyombo vya habari vinatumika kwa wakati moja kuandikia na kutangaza suala moja kupitia angle tofauti tofauti kwa kipindi cha wiki, wakati mwingine hata zaidi. Huu ni mkakati tuliouibua wakati tunapanga mipango iliyotupatia ushindi wa SOSPA. Matokeo yake ni makubwa , HAYANA KIFANI.

Kwa mtindo huo vile vile tumekemea na kuhamasisha jamii iachane na mila potofu, za kuwaoza kinguvu watoto wa kike katika umri mdogo kwa wanaume ambao wana umri mkubwa. Sifa nyingine kubwa kwa TAMWA, ni mafunzo ambayo tumeendesha kwa nyakati mbali mbali kwa wandishi wa habari ili waziandike kwa jicho la jinsia.

Tumepinga ukatili dhidi ya watoto, tumehamasisha wazazi na walezi wawapeleke watoto wa kike shuleni ili wapate elimu, maarifa na ujuzi vitakavyosaidia kuwapa mawanda mapana ya fursa zilizopo ili wafaidi Maisha yaliyo bora kwa ajili yao na watoto wao.

Hatimaye tumeelimisha, tumehamasisha na tutaendelea na harakati hizo tukiamini watoto wa kike na wakiume wakizifahamu haki zao za kijamii, kiafya na kiuchumi, wataweza kuzipigania na kuzitetea, na hivyo taifa letu kuondokana na umaskini ili maendeleo endelevu yatapatikane katika kipindi kifupi.

Wanaharakati wenzangu, TAMWA toka mwanzo iliamini sana katika kufanya utafiti kabla ya kushughulikia tatizo lolote lile. Kwa mfano, tuliona wengi wetu tumejengwa kuimba nyimbo za kikoloni kama vile London bridge is falling down au where are you going my pretty maid. Huu ni utamaduni wa wenzetu ambao waliuingiza katika lugha yao.

Baada ya kutafakari, tukaona haina mantiki sisi Watanzania na hasa watoto wetu kuendelea kuimba nyimbo zinazo upaisha utamaduni wa wenzetu wakati tuna nyimbo zetu nzuri zinazo akisi mandhari mazingira, hulka, malezi na mazoea yetu. Tunazielewa zinatuhusu na zina mantiki, nyimbo kama mabata madogo madogo yanaogelea katika shamba zuri la bustani, au maua mazuri yapendeza au kofia nyembamba nk .Tukamtafuta mwanamziki wetu , mdogo wake marehemu Patrick Balisidya ambaye alitutengenezea cassette nzima ya nyimbo za watoto ambazo tuliwapa RTD wakati huo wazitumie kuweka mahanjam katika vipindi vya watoto. Kwa Bahati mbaya cassette haipo lakini kitabu kipo. Vivyo hivyo, wakati huo, suala la madawa ya kulevya lilikuwapo japo si kwa ukubwa tunaoushuhudia leo.

Tulifanya utafiti na kuangalia kiini chake, madhara yake na kuandika machapisho kadhaa kuihadharisha jamii kuingia katika angamizo la kizazi cha sasa na kijacho kama hatutafanya kazi ya ziada kuweka sheria kali dhidi ya wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya. Waswahili wanasema mwanzo wa makubwa ni madogo na pia kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha. Kwetu TAMWA tulikemea, Tuliandika sana na kufanya vipindi kadhaa redioni. TV wakati huo ilikuwa Znz tu.

Baadhi ya machapisho hayo ni Sauti ya Siti, ambayo ni sauti ya wanawake. Tumekuza sana sauti za wanawake na watoto, kudai washirikishwe katika maendeleo ya nchi ili kero zao zitatuliwe na mchango wao uthaminiwe na kuheshimiwa, waweze kuishi Maisha yenye hadhi na yenye ustawi.

Haya ni baadhi tu ya mengi yaliyofanywa na TAMWA.

Wakati tunaendelea na harakati hizi, tukiwa na umri huu mkubwa wa miaka 30. tunawiwa kuchukua nafasi hii ya kipekee kabisa, kuwashukuru wote, hasa wandishi wa habari ambao mmetuwezesha kuwafikia watanzania kwa idadi kubwa kwa kipindi chote hiki. Kama usemi wa Misri unavyodhihiri wakati wakizungumzia umuhimu wa mto Nile kwa uhai wao, kwamba no Nile, no Egypt, na sisi TAMWA tunasema no media no TAMWA. Nadhani mnanielewa. Kupitia kwenu vyombo vya habari, uelewa wa jamii umeongezeka, utayari wao kukemea madhila haya tunauona, tunausikia na tunausoma.

Kwa ushahidi zaidi tena wa kisayansi, TAMWA, inafanya kazi na inaendelea kufanya kazi katika wilaya kumi kwa ufadhili wa DANIDA unaoitwa GEWE I & 2 toka Mwaka 2012. Wilaya hizo ni WETE, (PEMBA KASKAZINI ) UNGUJA MJINI MAGHARIBI,UNGUJA KUSINI, KISARAWE,NEWALA MTWARA,MVOMERO MOROGORO,LINDI VIJIJINI,RUANGWA LINDI, KINONDONI NA ILALA DSM. Wakati mradi unaanza, uelewa wa watu katika wilaya hizo ulikuwa 11% , baada ya miaka 2, utafiti uliofanywa ulionyesha ongezeko la 4% hadi kufikia 16%. Kwa jicho la haraka haraka tunaweza kusema asili mi anne ni ndogo sana lakini ni kubwa kwa kipindi kifupi cha miaka miwili kwani kadri tunavyoendelea kuhamasisha na kuwapa uelewa na mbinu za kuchukua hatua, tutaona mabadiliko makubwa zaidi. Nini siri ya mafanikio yetu?

Tunapenda pia kutamka wazi, kwamba kujitolea kwetu, nyakati zile kwa hali na mali, na ujasiri wetu kushughulikia masuala ambayo kijamii bado yalikuwa na hat leo tunaweza kusema yana ukakasi, kumetujengea uwezo wa kuendelea kutetea haki za wanawake na watoto katika mfumo wa kisayansi. Uwezo wa kuthubutu umekuwa nguzo madhubuti na yote tuliyofanya tuliyaamini na tulichukulia kazi hiyo kama wito kwa jamii. Sisi tumepata faida ya kuwa wandishi tuisaidie jamii kwa ujumla wake nayo ipaze sauti lakini zaidi tulilenga wale walio dhalili miongoni mwetu wakiwamo wanawake , walemavu na watoto.

 

HUKO TUENDAKO:

Masuala ya unyanyasaji , ukatili wa kijinsia bado yapo, na naweza kusema ukatili umepitiliza kiwango cha ubinadamu. Hata ukatili kwa watoto unazidi. Hapa nazungumzia ubakaji ulawiti, utumikishaji watoto katika mashamba, majumbani , kwenye madanguro, ukatili wanaofanyiwa watoto mitaani majumbani mwetu na ndugu zetu, marafiki zetu, wageni wetu na majirani pia.

Mengi ya matukio haya hayaripotiwi TAMWA inasikitishwa sana na jamii inayoishi karne ya 21 kukosa ujasiri wa kuripoti na zaidi kukosa uzalendo wa kutoa ushuhuda ili haki itendeke.Kama anavyosema Rais wetu Mh. Magufuli, rushwa inasababisha haki isitendeke na sote tunajua jinsi ambavyo baadhi ya wenye mamlaka wanavyopindisha sheria na kufanya mwenye haki aonekane mhalifu na mhalifu aonekane mwenye haki. Katika masuala ya ukatili na unyanyasaji rushwa imekithiri sana na ni kikwazo kikubwa sana katika kazi inayofanywa na TAMWA. Bila ushirikiano wa dhati kati ya familia zetu na vyombo vya dola, madaktari, walimu, majirani, madhehebu ya dini na serikali, matatizo haya ya kijamii hayawezi kuisha. Tutaendelea kujenga kizazi kiso maadili, kilichopondeka mioyo, kisichojiamini, kilichodhoofu kiafya, kiakili ambacho pia kitakuwa hakina mwelekeo.

Kituo cha usuluhishi na ushauri nasihi hapa TAMWA, kina uwezo wa kuwahudumia waathirika wa matatizo hayo, lakini hatuna mahali stahiki pa faragha ambapo mteja anaweza kujieleza kwa uwazi na kwa kujiamini. TAMWA inataraji kuweka jitihada zaidi katika kuwasaidia vijana hasa katika kukabiliana na tatizo jipya la ukatili wa kijinsia utokanao na matumizi ya ya mitandao, yaani internet. Tunawasaidia vijana ili wawe na mtazamo chanya katika Maisha yao na vizazi vyao. Wawe na mbinu za kutambua kupambana na ukatili huu mpya unaoendelea kukua kwa nguvu na kusambaa kwa haraka katika jamii yetu. TAMWA, inataraji kuongeza mawasiliano ya karibu na vijana kupitia kurasa za face book, instagram twitter na kuboresha tovuti yetu ya www.tamwa.org ili iwe na taarifa nyingi zaidi za muhimu kwa jamii hasa kwa kizazi kipya cha .com.

Kwa mantiki hiyo, lengo la mkutano huu, ni kuzindua harambee ya kuchangisha fedha ili tupate kituo cha kuwasaidia wahanga wa ukatili wa kijinsia ikiwezekana nchi nzima.

Aidha, tunaandaa kitabu kinacho akisi safari yetu ya miaka 30, yakiwemo mafanikio, matatizo, changamoto na mafunzo tuliyo pata katika kipindi chote hiki. Tuna mpango pia wa kutengeneza documentary ya kielectroniki itakayoelezea mengi zaidi kuhusu TAMWA.

Tuna imani kubwa Watanzania watatuchangia kwa hali na mali , ili haya tuliyopanga kufanya, yawezekane. Tunaomba tuwe sote katika mwelekeo wetu wa kutetea haki za binaadamu, kapinga ukatili dhidi ya wanawake, walemavu na watoto, ili TANZANIA yetu iwe na amani endelevu. ASANTE SANA KWA KUSIKILIZA.

 

NJIA ZA KUCHANGIA:

1. KWA NJIA YA TIGO PESA: -

Piga *150*01# OK

Chagua Lipia Bili

Ingiza Namba ya kampuni 606060

Weka Namba ya kumbukumbu 606060

Ingiza Kiasi kisha namba yako ya siri kukamilisha.

Jina la kampuni ni TAMWA

 

2. KWA NJIA YA BENKI:

Jina la Bank CRDB

Account namba: 01J2027600600

Jina la Account: TAMWA

 

Kwa maelezo zaidi tupigie simu namba 0222772681 au 0222771005 TAMWA.

TAMKO LA KUZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 30 YA TAMWA - TAREHE 30 AGOSTI 2017.

Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Redio One, Bi Joyce Mhaville akizindua rasmi wiki ya maonyesho kuelekea siku ya maadhimisho ya miaka 30 ya TAMWA

UZINDUZI WA WIKI YA MAONYESHO MIAKA 30 YA TAMWA

Baadhi ya kazi za mikono za wanawake wajasiriamali katika wiki ya MAONYESHO kuelekea kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 30 ya TAMWA.

WIKI YA MAONYESHO KUELEKEA MIAKA 30 YA TAMWA

Ndugu Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari Wanawake nchini TAMWA,

Mkurugenzi wa TAMWA,

Board ya TAMWA

Wanachama wa TAMWA

Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali.

Habari za asubuhi!

 

Nafurahi kuwepo na ninyi hapa leo katika ufunguzi wa wiki ya maadhimisho ya miaka 30 ya kuanzishwa kwa TAMWA. Hongera sana Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA

 

Pia pokeni salamu nyingi kutoka kwa wafanyakazi wote wa ITV/Radio One !

 

Kwa ujasiri kabisa,

Ningependa kueleza furaha yangu kwa kujumuika na nyinyi siku hii ya leo katika kuzindua wiki ya maadhimisho ya miaka 30 ya chama cha  TAMWA.

 

Ndugu Waandishi wa habari

TAMWA ni chama maarufu kinachojulikana sana  hapaTanzania pamoja na nje ya nchi siyo tu kwa kuanzishwa miaka 30 iliyopita bali kwa uwezo na mafanikio yake katika utetezi na ushawishi  wa masuala yanayoendana na dhima yake.

Inakumbukwa na wengi hadi leo jinsi chama cha  TAMWAkilivyosimama kidete mwaka 1998 kuwahamasisha waheshimiwa wabunge kule Dodoma katika kutunga sheria ya makosa ya kujamiiana na kule Zanzibar ambako pia kiliweza kulishawishi balaza la wawakilishi kuibadilisha sheria ya mwaka 1985 ambayo mtoto mwari akipata ujauzito alikuwa akifungwa miaka miwili. Hayo ni mafanikio makubwa katika upande wa ushawishi na utetezi.

 

Kwa muda wa miaka 30, TAMWA imejikita zaidi katika kutimiza dira yake ambayo ni Tanzania yenye amani inayoheshimu haki za binadamu kwa mtazamo wa kijinsia. Ili kufanikisha dira hiyo, shughuli mbalimbali zimekuwa zikifanyika kwa pande zote mbili – Tanzania Bara na Zanzibar.

TAMWA imeiwezesha jamii mbali mbali hapa nchini kuongea kwa uwazi kuhusu ukatili wa kijinsia na vitendo hivyo kuvichukulia harua za kisheria pale inapotakikana.

TAMWA imekuwa na ushirikiano wa kupigiwa mfano na vyombo vyote vya habari hapa nchini.

Hayo yote myafanyayo yamo katika vipaumbele vya Serikali. Kwa hiyo, tunapenda TAMWA ifahamu kuwa jamii inathamini sana mchango wenu katika kujenga jamii huru na yenye kuthamini mchango wa wanawake katika  kufikia malengo ya mipango na mikakati ya serikali ya awamu ya tano chi ni ya Mheshimiwa  Rais Dr John Pombe Magufuli.

Kwa namna ya pekee ITV na Radio One inatoa pongezi za dhati kwa juhudi za TAMWA kwa kuongeza usawa wa kijinsia hapa nchini. Halikadhalika ITV na Radio One itaendela kutoa ushirikiano na TAMWA katika kuelimisha jamii kuhusu usawa wa kijinsia na kupiga vita aina zote za ukatili wa kijinsia.

ITV na Radio One inatambua kwamba TAMWA ina dhamira ya  kujenga na kuendeleza kituo chake kwa lengo la kuongeza huduma za ushauri nasihi pamoja na msaada wa kisheria kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia. Napenda kukuhakikishia ndugu Mkurugenzi wa TAMWA, kwamba sisi ITV/Radio One tupo pamoja nanyi tutajitahidi kadri ya uwezo wetu kutoa usaidizi ili kutimiza dhamira yenu njema na yenye faida kubwa kwa jami yetu.

Ndugu washiriki wa maonesho haya, Fursa hii ya maonesho ni muhimu sana kwani inatuongezea uelewa na hata kutupa huduma mbalimbali bila ya gharama ikiwa ni pamoja ushauri nasihi, huduma za kisheria, huduma za afya na maarifa mbalimbali yatakayo fundishwa katika semina zilizo andaliwa ikiwa ni pamoja na masuala ya Ujasiriamali, Misingi ya uandishi wa habari na athari za ukatili wa kijinsia.

Mwisho nawatakia maonesho mema na yenye tija kwa wote.

Na kwa heshima kubwa Nazindua wiki ya Maadhimisho ya Miaka 30 ya TAMWA. 

HOTUBA YA UFUNGUZI WA MAONESHO YA MIAKA 30 YA TAMWA 14th  Nov. 2017

Siku kama ya Leo Miaka 30 iliyopita, kilizaliwa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA). Katika kuazimisha siku hii, Leo tutakuwa na Tukio la KUCHANGIA Ujenzi wa Kituo cha Ushauri Nasihi, Saikolojia na Msaada wa Kisheria kuanzia SAA 12 Jioni hadi SAA 4 Usiku katika Ukumbi wa Kisenga LAPF International Conference Center (KLICC) ulipo Kijitonyama jengo la Millenium Tower.

   Mgeni Rasmi ni Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe.

   Tafadhali Tuma Mchango wako:

   TIGOPESA Malipo weka namba ya kampuni/kumbukumbu 606060

   MPESA Malipo weka namba ya kampuni/kumbukumbu 370077

   ***Mkono Ubebao Mwana ndio Uleao Taifa***

HAPPY 30th ANNIVESARY TAMWA

Dr.Harrison Mwakyembe akizindua Kitabu kinachoelezea Historia ya Miaka 30 ya TAMWA

UZINDUZI WA KITABU CHA MIAKA 30 YA TAMWA

Dr.Harrison Mwakyembe akizindua TAMWA Online TV itayokuwa ikirusha kipindi cha Sauti ya Siti ambacho kinaakisi maisha halisi ya wanawake, watoto na makundi maalumu na changamoto wanazokutana nazo katika jamii

UZINDUZI WA TAMWA ONLINE TV

 

TAMWA 30 YEARS ANNIVERSARY

As we approach 30 years on media advocacy, TAMWA aims to collect funds for building an expanded and improved Crisis Resolving Centre to provide free service to Gender Based Violence (GBV) Survivors majority of whom are Women and Children. Join hands with TAMWA, Say NO to GBV. Send your donation via below accounts;

  1.   VIA BANK        - Bank Name:             CRDB

                                      - Account Number:    01J2027600600

                                       -Account Name:         TAMWA

  1. TIGO PESA         *150*01# OK, Choose Bill payment;

                                       - Bussiness Number:   606060

                                       - Company number: 606060

                                       - Company Name:     TAMWA.

  1. M PESA            *150*00# OK, Choose Pay by Mpesa;

                                      - Bussiness Number:   370077

                                      - Company number: 370077

                                      - Company Name:   TAMWA.

       4. YOU CAN ALSO DELIVER US A CHEQUE AT OUR OFFICE LOCATED AT SINZA MORI, DAR ES SALAAM.

For more information call our numbers  0222772681 or 0222771005

 

 

OUR YOUTUBE VIDEOS

Visitors Counter

1392807
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
1029
2907
6428
1369172
30142
1733
1392807

Your IP: 54.145.124.143
2017-11-21 07:53

Events - Calendar

November 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

FOLLOW US ON FACEBOOK

Map

JoomShaper